Huduma zilizopo kwa Gurudumu – Guka la Ziara Moja

Nakala imeandikwa na Manya Andrews

Ni asubuhi mapema katika zahanati ya Mwala ilio mkoa wa mashariki nchini Kenya, na popote uangaliapo, wanawake na watoto wamejaa kwenye ubao unaoning’inia. Akina mama wameshika na kuwatuliza watoto wachanga, wakipanga mablanketi na kofia zenye rangi nyingi, pale watoto wengine wameinama karibu na nguo za mama wao zenye rangi angavu. Wengi wa wanawake hawa wamesafiri mbali kuleta watoto wao kupata chanjo na wanatazamia kungojea siku nzima katika chumba hiki ambacho kimejaa.

Kwa sababu yoyote ile, akina mama kuwako hapa yaonyesha umuhimu wa kuendeleza mradhi wa afya unaojishugulisha na mshiriki na unao uunganisho. Hii ni nafasi ya kutoa huduma kamilifu iwezekanavyo: elimu ya kulisha vyema, unyonyeshaji na kuachisha kunyonya, ushauri na upimaji wa Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV); huduma za upangaji familia; upimaji saratani ya shingo ya kizazi na mengine mengi.

Wauguzi wawili walio na kazi nyingi hufanya wawezao kuhudumia umati huu mpaka gari kubwa nyeupe inafika, ikivuruta gari la kufungashia nyuma ya gari lingine, lilio na sanduku la fumbo. Kundi kutoka hospitali ya wilaya ya Kitui linaasili na zahanati ilio kwa magurudumu – duka la ziara moja ambalo lina utunzaji mzima linaowapa wagonjwa faragha na wenye maarifa wa matibabu kutibu magonjwa yao.

“Gari hili la afya lenye magurudumu” ni mojawapo wa mambo mapya na ya akili katika uendeleshaji wa afya ya jamii chini ya mradhi wa UKIMWI (AIDS), Idadi ya Afya ya watu na Kipangama cha Usaidizi II wa Mradhi wa Mashariki (A2E), uliosaidiwa na Wakala wa Marekani wa Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na kusimamiwa na Jhpiego ikishirikiana na washirika watano na serikali ya Kenya. Uzushi huu uliundua kuvutia na kuweka washiriki wengi iwezekanavio kwa kuwasaidia na mahitaji yao ya afya katika ziara moja tu.

Nafasi Zisipotezwe

“Kwa sababu ni ngumu sana katika mkoa wa mashariki kufika kwa zahanati, wagonjwa wakija hapa, wanatarajia kila kitu kufanywa,” aeleza daktari Leonard Okoko, afisa wa huduma za matibabu aliye wilayani Kitui. “Tunapowatuma kwenda vituo vingine vilio mbali kupata huduma kama upangaji familia, hawaendi – na wanapata watoto kila mwaka/wanashika mimba kila mwaka.”

Kusuluhisha tatizo hili, kundi hili la serikali la kufikia walio mbali wana shabaha zahanati zilizotengwa zinazohudumia umati mkubwa wa watu katika maeneo ambayo chanjo na utumiaji wa huduma za upangaji familia ni lengevu,” anasema. Wenye maarifa ya kulisha, madaktari wa magonjwa ya wanawake, wauguzi, madaktari wa dawa, afisa wa wilaya wa afya ya umma na kundi la Kipangama cha Usaidizi II wa Mradhi wa Mashariki (A2E) wanapanga wiki nyingi mbele ya kufika ili kutayarisha zana na duka lenye mwendo la dawa. Wanafanya kazi na mjumbe wa janibu, watoaji utunzi wa afya wa jamii kueneza habari juu ya tarehe ya kufika na huduma zitakazotolewa huko.

Kundi likiwasili kwa kituo, linatengeneza pahali litakapofanyia kazi kwa urahisi na kupanga kazi ya kila mtu. Wanatumia kama zahanati, hema, makanisa, miskiti, shule na kadhalika kama vituo vya kutoa huduma. Kundi lina wenye maarifa ya mambo kama ushauri wa kulisha, ushauri na upimaji wa Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV) upangaji familia na suluhisho za shaka kadhaa wa kadhaa za afya.

Kazi ya kundi inalinganisha vyema huduma mbalimbali na chanjo, upimaji na matibabu ya kifua kikuu, matibabu ya kinga virusi lakini bado kuna mwanya.

“Upangaji familia bado ni tatizo,” asemae Okoko. “Hawa ni watu ambao wanahitaji njia za muda mrefu – kifaa cha mfuko wa uzazi wa ndani (IUD) na zingine za kutia ndani imara. Haifai watembelee zahanati kila miezi mitatu kupewa huduma za muda mfupi. Tunaweza kufanya madogo tukiwa na pazia na hema tu. Hizi ni taratibu za ndani ambazo zinazohitaji maficho.”

Yawezekanaje vyema na kwa busara? Jibu lilionekana wakati daktari Kenneth Chebet, mkurugenzi wa Kipangama cha Usaidizi II wa Mradhi wa Mashariki (A2E) alipoona gari ndogo liliojengewa na mwenyewe na kutengwa. Daktari Chebet aliuliza kampuni iliojenga gari lile ijenge gari la afya la kufungashia nyuma ya gari lingine.

Daktari Ruth Jahonga, daktari mwenye maarifa ya ukunga wa kundi la Kipangama cha Usaidizi II wa Mradhi wa Mashariki (A2E) anasema gari la afya la kufungashia nyuma ya gari lingine limegeuza kazi yake sana. “Kwanza, tuna pahali pa kutosha pa kuweka zana tunazohitaji. Ya pili, kwa sababu zana zinakaa katika gari, tunaweza kuzuia na kulinda zana zetu vyema.”

“Walakini jambo lilio njema,” anasema, “ni vile gari limegeuza utoaji huduma kwa washiriki. Kwanza, walikuwa na tunu lakini sasa wakiingia kwa gari, wanacheka. Ni safi, halina joto na lina amani. Ninawaona wakiwa na faragha na wanaweza kueleza matatizo yao bila wasiwasi matatizo yao watajulikana na jamii yote. Wanaeleza kwa ukweli juu ya mienendo yao ya mapenzi na tunaweza kuwapa utunzi na ushauri wa kufaa,” anasema Jahonga. “Wakitoka wana furaha, wanawaambia rafiki zao wanaongojea ya kwamba utunzi ni mwema – wanatarajia kurudi kwenya gari!”

Shida lilio na gari hili ni vile ni moja tu.

“Ninanuia yangekuwa mitano hapa mkoa wa mashariki,” anasema Okoko. “Ingawa tulikuwa na magari mengi yanayofanyizwa kazi kila siku, tungesaidia sana. Tungeyapeleka kila pahali – bila tu kwa vituo. Tukiwa na msafara, tungekuwa na zahanati popote……..”

Copyright © 2000-2012 Jhpiego Corporation. All rights reserved.
Web Policy | Site Map | E-mail Us