Afya ya Mama, Watoto Wachanga, na Watoto kwa Jumla

Jhpiego, ambalo ni shirika la afya la kimataifa na ambalo ni mushiriki wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, limekuwa likifanya kazi ya kuleta hatua hizo za kuokoa maisha ya akina mama na watoto wachanga duniani kote kwa zaidi ya miongo mitatu. Tangu mwaka wa 1998, tumekuwa tukiongoza miradi ya Shirika  La Maendeleo ya Kimataifa la Marekani ili kuwaongezea wajawazito na watoto wachanga afya na maisha: mwanzoni, Afya ya Wajawazito na Watoto Walio Chini ya Mwezi mmoja - MNH (1998-2004), na kwa sasa, Upatikanaji wa Hospitali kwa Jumuiya ya Wajawazito , watoto chini ya mwezi moja na mradi wa shirika la Afya ya Wanawake  “Neonatal and Women's Health Services (ACCESS) Program (2004-2010)”; shirika la kimataifa la ACCESS linalohusu Mpango wa Uzazi (2005-2010) na kuanzia mwaka 2008 na kuendelea hadi 2013, mradi wa Afya ya Watoto na Wajawazito "Health Integrated Program (MCHIP)". Kama mojawapo ya wanaoongoza katika miradi hii ya kimataifa, Jhpiego ina nafasi muhimu katika kuongoza juhudi za dunia kuelekea kufikia lengo la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Milenia la kupunguza maradhi na vifo vya wajawazito na watoto wachanga.

Wanawake wenya Afya ndio msingi wa jamii zenya nguvu, na watoto wenye afya ndio jamii ya kesho. Hata hivyo, kila mwaka zaidi ya wanawake 500,000 hufariki kutokana na matatizo ya ujauzito na wakati wa kujifungua, na wastani watoto wachanga milioni nne hufariki katika mwezi wa kwanza wa maisha yao.1Idadi kubwa ya vifo hivi hutokea katika nchi zinazoendelea,1 ambapo huduma za afya zinazofaa mara nyingi hazipo au hazipatikani kwa urahisi—na kufanya wanawake wengi kujifungua watoto katika vituo visivyo na huduma au vifaa vya kutosha, pamoja na kujifungua nyumbani bila ya kuwa na watoa huduma wenye maarifa. Kuongezea kwenye upotevu huu wa kuhuzunisha wa maisha ni kuwa sababu kubwa inayosababisha vifo hivi vya ujauzito na watoto wachanga kabisa na ulemavu zaweza kuzuiwa au kusimamishwa  kwa kutumia hatua  zisizo na gharama kubwa ambazo zimethibitishwa kuokoa maisha.

Jhpiego Inachofanya

Jhpiego ina mipango ya afya ya uzazi na watoto wachanga katika nchi zaidi ya 25 katika Afrika, Asia na Amerika ya Kusini. Kupitia juhudi2 hizi zinazoendelea, tunashirikiana na wizara za afya na mamia ya mashirika ya kimataifa kwa juhudi za kushughulikia vikwazo dhidi ya  matolezi ya huduma za afya za hali ya juu kwa wajawazito, watoto wachanga na watoto kutoka kwenye kaya hadi hospitalini. Ushirikiano wetu unalenga mapanuzi mbalimbali ya umuhimu wa kiufundi—kutokana na utaalamu wetu katika uzalishaji/gynecologia, ukunga na afya ya watoto wachanga—ikiwa ni pamoja na:

  • Kuongeza upatikanaji na matumizi ya watu wenye ujuzi wa kutoa huduma ya uzazi na kwa watoto wachanga—mojawapo ya uingiliaji muhimu katika uokoaji wa maisha

Uunganishaji wa huduma mbalimbali kwa ajili ya kuboresha matokeo ya wajawazito na watoto wachanga katika jukwaa la huduma ya "focused antenatal care", ambayo inakuza huduma za msingi ambazo zinaweza kupeanwa kupitia ziara nne kwenye zahanati angalau

  • Kuongezea upatikanaji na matumizi ya huduma zilizo za msingi ili kusaidia kwa kila dharura uzalishaji na watoto wachanga (basic and comprehensive emergency and newborn care), ili kuhakikisha kwamba takriban 15% ya waliozaliwa na matatizo kuweza kutambulika na kusimamiwa kwa haraka
  • Utoaji wa habari na huduma za mpango wa uzazi katika kipindi cha "postpartum", hii ni hatua nyingine ya kuokoa maisha, na huwa ina uwezo wa kufikia zaidi ya 90% ya wanawake wa umri wa uzazi kwa vipimo vya juu vya uwezo wa kuzalisha.
  • Uzuiaji na tiba ya malaria wakati wa ujauzito, hii ni kushughulikia sababu kuu ya vifo vya wajawazito na watoto wachanga katika nchi zilizo na hatari hii
  • Kuzuia uambukizanaji wa  Virusi vya Ukimwi kutoka mama-kwenda-kwa mtoto, ili kusaidia kuzuia sababu kubwa ya Virusi vya Ukimwi/Ukimwi kwa watoto
  • Kuzuia na matibabu ya ugonjwa wa kuvuja damu (postpartum hemorrhage); "prolonged/obstructed labor", sababu kubwa ya "obstetric fistula"; na "pre-eclampsia/eclampsia" ikilenga baadhi ya sababu zinazoleta vifo vya watoto wachanga na wajawazito zinazoweza kuzuiliwa kwa urahisi na ambazo hutokea mara kwa mara
  • Kuongeza upatikanaji na matumizi ya huduma za hali ya juu kwa watu waliotoa mimba ili kuzuia vifo vya kutokana na matatizo ya mimba
  • Uboreshaji wa huduma na shughuli za kuzuia maambukizi kwa minajili ya kusaidia uzuiaji wa "postpartum" na magonjwa ya watoto wachanga.

Kufanya Kinachofanya Kazi Kifanye Kazi

Hatua za kiufundi ambazo Jhpiego inakuza zina uwezo wa kuokoa maisha ya watu wengi. Hata hivyo, ni lazima hatua hizo kutolewa na watoa huduma za afya ambayo wamehitimu kabisa katika mazingira ya mfumo wa afya unao matokeo —moja wapo ikiwa ni kuwaadili  wateja wake na daima kuzidi kutambua na kutoa huduma za hali ya juu. Kwa minajili ya kuanzisha muktadha huu, Jhpiego imeweza kufanya kazi kwa karibu na wizara za afya, watunga sera na wadau wengine wa mtani ili kutekeleza mbinu bunifu katika maeneo yafuatayo:

  • Kujenga mazingira bora ili kuboresha mifumo ya afya kwa njia ya maendeleo ya sera na miongozo
  • Kuimarisha rasilimali kwa ajili ya elimu na mafunzo ya watoa huduma za afya
  • Kutekeleza mpango unaohusisha viwango vya msingi na kuboresha utendaji na ubora wa wafanyakazi wa afya na vifaa vyao.
  • kutumia mbinu zinazo husu jamii na kuwawezesha wananchi kuwa washiriki katika huduma ya afya zao.

Kupitia kazi yetu katika afya ya wajawazito na watotowachanga, kama kawaida ya juhudi zetu zote, Lengo la muhimu zaidi la Jhpiego’s ni uendelevu, kuhifadhi mtandao ulio tayarishwa vyema wa waatalamu wa huduma za afya na pia msingi imara wa kitaasisi  ili waweze kuuendeleza wakati tutakapoondoka.

1Save the Children. 2008. Stateof the World’s Mothers 2008: Closing the Survival Gap for Children Under 5.
2Kutumia uhifadhi kutoka kwaUSAID; mashirika ya kimataifa, kama Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID), UNICEF na Shirika la Afya Duniani; na mashirika ya Kibinafsi na pia misingi, ikiwa ni pamoja na ExxonMobil na  MacArthur Foundation.

Haki © 2000 Jhpeigo ni shirika la chuo kikuu cha Johns Hopkins. Haki zote zimewekwa

Sera ya tovuti  | Ramani ya tovuti | Maoni