Afya ya mijini na jumuiya

Ufafanuzi

Jhpiego, ambayo ni shirika mojawapo wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, imefanya kazi nchini Kenya kwa miaka 35 ili kuboresha afya na ustawi wa wanawake na familia zao. Tangu mafunzo ya mwanzo ya Jhpiego yaliyofanyika Kenya katika miaka ya mwanzo ya miaka ya 1970s, Jhpiego imeanzisha mbinu fumbuzi zilizo lengwa kutimiza mahitaji mbalimbali ya wakazi nchi kote.

Lengo muhimu na linalozidi kutiliwa maanani na Jhpiego ni afya ya wakenya ambao wanaishi katika makazi ya mjini yasiyo rasmi, yanayojulikana kwa kiingereza kama "slums". Kwa sababu ya  changamoto ja kijamii kama  vile kunyimwa haki, na usalama duni, kati ya nyinginezo, jamii hizi huwa na mahitaji ambayo hayapatikani kuhusiana na afya ya uzazi, Virusi vya Ukimwi/UKIMWI na huduma nyinginezo za afya, licha ya kuwa kati ya sehemu ya miji iliyo na maendeleo. Ikihifadhiwa na Msingi wa Rockefeller na "Wallace Global Fund", mradi wa Jhpiego wa mijini ni kuhakikisha ya kuwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi kwenye sehemu za Nairobi za Korogocho na Viwandani wanapata huduma za afya zenye upana wa huduma za kimwili na kisaikolojia.

Mafanikio na Suluhisho

Mbinu za Jhpiego za kuunganisha watoa huduma za afya na jamii wanazozihudumia umefanikiwa zaidi. kwa kufanya kazi na watoa huduma za afya na wakazi wa makazi haya duni ili kutambua na kushughulikia mahitaji yao, Jhpiego imezihamasisha jamii za Korogocho na Viwandani ili kuendelea kutafuta njia za kuibunisha upatikanaji wa huduma ya afya.

Jhpiego imewafunza zaidi ya watoa huduma za afya 200 wenye msingi wao katika makazi haya duni ambao wanawahudumia zaidi watu 120,000 walio wateja wao. Jhpiego pia imeandaa na kutenga siku za maelfu ya wakazi wa jamii hizi , wakiwemo watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, ambao hawapewi tu huduma za afya za  papo hapo—kama vile ushauri nasaha wa hiari na upimwaji, chanjo kwa watoto na upangaji uzazi—lakini pia wanaagizwa usaidizi wa kisaikolojia, kisheria na/au  kiroho.

Mafanikio ya kikweli ya mradi huu katika makazi duni yamekuwa sana kutokana na kukubaliwa kwa wingi na jamii, na mara nyingi kusambaza matokeo ya mradi huu mbali zaidi ya upeo wao wa asili. Kwa mfano, Vijana wakufunzi wa rika waliofunzwa na Jhpiego ili kuwapa shauri rika zao, kuhusiana na njia salama ya afya ya uzazi na pia njia salama ya ngono walifanya kazi katika jamii zao ili kupunguza vurugu  zilizofuatilia uchaguzi wa Januari 2008.  Wakufunzi hawa wa rika waliokoa maisha kwa kutumia ujuzi walioujifunza kupunguza  mvutano na kudumisha amani. Kundi lingine limeanzisha shirika mpya lisilo la kiserikali liitwalo "Expert Patient Trainers International," ambalo limeundwa na wagonjwa wataalamu ( "expert patients”)—watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi—ambao hutumia mazoea yao binafsi ili kuwafunza watoa huduma za afya jinsi ya kutoa huduma zenye nyeti zaidi, zinazo lenga huduma kwa mteja aliye na Virusi vya ukimwi.

Kutazama Jinsi Mwelekeo wa Jhpiego’s Unavyofanya kazi:

Kuunda Mtandao Rufaa (Referral network)

Ikishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali na  mashirika yaliyo na Msingi wa kidini, Jhpiego imeongoza katika juhudi za kuunda mtandao mkubwa wa rufaa ili watoa huduma waweze kuwaelekeza wateja kwenye vituo sahihi vya afya, na ili wanaoishi kwenye jamii hizi waweze kupata huduma wanazozihitaji kwa urahisi. Utaratibu huu wa kuendeleza mtandao rufaa ulio na matokeo unahusisha sehemu tatu muhimu zifuatazo:

Kuelimisha na kuwapa uwezo  wateja na jamii—Jhpiego huunganisha wakazi wa jamii na huduma mbalimbali za afya, na kuwapa uwezo kujiendeleza na kuongezea elimu yao juu ya afya yao huku wakisaidia kukabiliana na unyanyapaa katika jamii zao, hasa kwa watu walio na Virusi vya Ukimwi. Huduma hizi ni pamoja na: ushauri na kupimwa Virusi vya Ukimwi; tiba ya kurefusha maisha; huduma za afya ya kizazi kama vile mwongozo wa upangaji uzazi na ushauri kwa wanawake wajawazito na watoto wenye Virusi vya Ukimwi; elimu ya lishe; chanjo; kuhusishwa na vikundi vya kusaidiana; na ushauri juu ya haki za kisheria kwa watu walio athirika na Virusi vya Ukimwi.

Kufunza na Kuwaanda watoaji huduma—Ili kudumisha mtandao rufaa ulio na mafanikio, madaktari, wauguzi, wakunga na watoa huduma za afya kwa jamii wanaofanya kazi kwenye makazi duni lazima wawe tayari kuwapokea wateja. Watu walio na Virusi vya Ukimwi wanaoishi kwenye makazi  duni wanakabiliwa na changamoto aina nyingi, kama vile unyanyapaa na kubaguliwa na familia, marafiki na pia wenzao; ukosefu wa lishe bora; na ukosefu wa kijumla wa maswala kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi. Wakazi wengi wa jamii hizi pia hukosa elimu juu ya mpango wa uzazi na huduma za afya ya uzazi. Jhpiego  imetengeza kwa makini, mpango wenye upana ambao unaimarisha uwezo wa kiufundi wa watoa huduma na uwezo wao wa kushughulikia haja hizi za kipekee na kuongezea upatikanaji wa huduma za afya za hali ya juu.

Kuweka Vifaa kwenye Vituo—Jhpiego imeboresha huduma zinazotolewa katika vituo vya afya kwa kuzikabidhi vifaa vya kuzuia mambukizo ya kawaida kwa kutumia vifaa kama "disinfect-ants", sabuni,glovu,ndoo,mifuko ya kutupa takataka,besheni,na taulo za binafsi za mikono. Wafanyakazi wamefunzwa jinsi ya kutunza na kubadilisha vifaa hivi ili wateja wote waweze kupata vituo vya afya vilivyo safi, salama na zinazotoa huduma.  Vifa vya kuchoma vitu pia zimeundwa katika vituo hivi ili kuzuia mambukizi.

Kupiga Hatua Mbele

Tatizo hili la  kutoa huduma za hali ya juu kuhusiana naVirusi vya Ukimwi/UKIMWI na afya ya uzazi katika makazi duni ni lakuogopesha kwa wateja na pia watoa huduma. Ikiendeleza juu ya historia yake ya kuongezea ufumbuzi na vitendo tekelevu, na kupitia mpango wake mbainifu wa mahusiano ya jamii  na vituo,  Jhpiego i tayari kuongezea mafanikio yake katika makazi duni katika sehemu zingine za Kenya na sehemu  nyingineko.

Haki © 2000 Jhpeigo ni shirika la chuo kikuu cha Johns Hopkins. Haki zote zimewekwa

Sera ya tovuti  | Ramani ya tovuti | Maoni