Jhpiego: Historia

Kujibu Mahitaji Yanayobadirika ya Wanawake na Jamii Duniani

Tangu ilipoundwa mwaka wa elfu moja mia kenda sabini na nne (1974), Jhpiego imegundua jinsi ya kuhifadhi maisha ya wanawake na jamii duniani. Kutoka siku ya kwanza, Jhpiego imeuliza swali hili: “tunawezaje kufikisha huduma za kuhifadhi maisha ili ziwakaribie wanaozihitaji duniani kote?”

Daktari Theodore M. King, mzuzi wa mapema na mjusi wa afya ya kina mama, alikuwa shujaa mmoja wa waundaji wa Jhpiego. Jhpiego ni shirika la chuo kikuu cha Johns Hopkins. Miaka ya kwanza ya mwongo wa miaka ya elfu moja mia kenda na sabini (1970s), Daktari King alitambua haja ya madaktari, wauguzi na wasimamizi wa afya wa nchi zinazoendelea kufahamu maendeleo katika afya ya uzazi kama Laparascopy (utaratibu wa kuchunguza uwezo wa uzazi wa viungo vya ndani ya mwili vya uzazi au kuzuia uzazi kwa kufunga bomba za wanawake za uzazi). Mbeleni, ilijulikana kama programu ya masomo ya kimataifa ya magonjwa ya wanawake na maarifa ya ukunga ya Johns Hopkins, shirika lililoundwa na usaidizi kutokana na shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Udharua wa Marekani (MKUM). Chini ya uongozi wa Daktari King aliye mundaji, mdhamini na msimamizi wa Jhpiego muda wa miaka kumi na minne, shirika lilifanya kazi nyingi thabiti dunia ya nchi zinazoendelea.

Tulitokaje hapo kuja hapa?

Mwanzoni, Jhpiego ilijiimarisha kuwa kiongozi katika elimu ya afya ya uzazi. Kwanzia mwaka wa elfu moja mia kenda sabini na nne (1974), Jhpiego ilifundisha madaktari na wauguzi upangaji uzazi/afya ya uzazi nchini Marekani. Mwaka wa elfu moja mia kenda sabini na tisa (1979), Jhpiego ilianza miradhi ya masomo katika nchi za Tunisia, Brazili, Kenya, Nijeria, Thai na Filipino. Kutoka mwaka wa elfu moja mia kenda themanini na tisa (1989) hadi mwaka wa elfu mbili na nne (2004), Jhpiego iliendelesha miradhi mitatu ya ulimwengu ya masomo ya afya ya uzazi iliofadhiliwa na Maendeleo ya Kimataifa ya Udharura wa Marekani (MKUM). Kwanzia mwaka wa elfu moja mia kenda tisini na tatu (1993), Jhpiego ilichapisha maandiko ya kuelimisha juu ya utaratibu wa upangaji uzazi.

Miaka ilipita,Jhpiegoikaanza ofisi za uga ili kuitikia mahitaji ya mojawapo ya nchi. Ofisi ya kwanza ya uga ilifunguliwa nchini Kenya mwaka wa elfu moja mia kenda tisini na tatu (1993). Leo, Jhpiego ina ofisi za uga katika nchi zaidi ya thelathini duniani. Vile vile, eneo ambazo Jhpiego hufanya kazi zimeongezeka kupatana na mahitaji yalioko miongoni mwa wanaosaidiwa. Zaidi ya upangaji uzazi na afya ya uzazi, leo Jhpiego ina ustadi wa afya ya mama na watoto, pinzani ya uambukizo, Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (VVU)/Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI) na magonjwa yanayoambukiza. Kazi ya Jhpiego imepanuka kujishuhurisha na sera na miongozo ya afya ya uzazi ili kutegemeza mifumo ya afya. Kwa mfano, mwaka wa elfu moja mia kenda tisini na sita (1996) nchini Brazili, Jhpiego ilianzisha uelekezo wa kupima tendo na ubora unaojulikana kama Usimamizi wa Viwango vya Msingi na Utambulisho (SBM-R), na sasa umetekelezwa katika nchi thelathini. SBM-R inawezesha wafanyakazi wa afya urahisi wa kusitawisha tendo na ubora wa huduma zao kwa kuwapa vyombo na utaratibu wanaohitaji ili kukata shauri, kutatua matatizo na kugeuza mambo ya janibu.

Uzushi wa Taratibu za Elimu,Teknolojia

Mwaka wa elfu moja mia kenda themanini na sita (1986), Jhpiego iliongoza njia ya elimu yenye nguvu ambayo ina dhihirisha elimu ya kutenda. Mbinu hizi zina kaza namna washiriki wanatekeleza na kuendelesha uwezo wa mwalimu kushawishi elimu. Jhpiego ilianzisha pia utumiaji wa vifani vya miili ili kuwezesha elimu ya maana. Kupunguza hatari kwa washiriki, wanafunzi hutenda mara kwa mara na vifani mpaka wapate ustadi. Mwaka wa elfu moja mia kenda tisini na tano (1995), kitabu kidogo cha uelimishaji wa ujuzi wa zahanati, jiwe la pembe ya utaratibu wa funzo ya Jhpiego kilichapishwa. Kwa kutumia utaratibu wa ‘funzo la wakufunzi’, Jhpiego imeunda wavu wa ulimwengu wa wataalamu wa madaktari, wauguzi na wakunga.

Vile vile, mapema mwaka wa elfu moja mia kenda themanini na nne (1984), Jhpiego iliungana na chuo kikuu cha West Indies kupa kozi ya afya ya uzazi kwa njia ya setilaiti, kwa viziwa sita katika bahari la Karibiani. Mwaka wa elfu moja mia kenda themanini na saba (1987), mkutano wa ulimwengu wa elimu ya afya ya uzazi na teknologia ulidhaminiwa na Jhpiego pamoja na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO). Jhpiego ilianzisha elimu inayoendelezwa na compyuta kusaidia hali ya zahanati katika mifulizo kadhaa ya Marekani.  Mwaka wa elfu moja mia kenda tisini na tano (1995), Reproline, chimbuko la mtandao ya maelezo ya afya ya uzazi ilianzwa. Leo, Jhpiego inaendelea kutafuta teknolojia mpya ya kufunza; simu za mkono nchini Afuganistani, masomo ya udhibiti wa mifumo kupitia compyuta huko Uhabeshi na Ghana na programu ya masomo ya mbali nchini Zambia.

Ufumbuzi wa Kufaa Makaoni bila Mitaji

 Tangu chapisho ya kanuni kumbukumbu Uzuiaji wa Uambukizo kwenye Programu za Upanganji Uzazi mwaka wa elfu moja mia kenda tisini na mbili (1992), Jhpiego inatangulia katika endelezo ya mazoezi ya ushahidi kulinda wafanyakazi wa utunzaji afya na pia washirika kutokana na uambukizi wa maradhi maishani. Kuelekeza haya, Jhpiego imechunguza na kuanza namna za taratibu za uzuiaji zisizo za gharama ya juu ambazo zinaweza kutumiwa viema katika mahali pasipo na mitaji.

Katika nchi zinazoendelea, saratani ya shingo ya kizazi ni moja ya sababu tangulizi za kifo kwa vifo vya saratani kwa wanawake. Mwaka wa elfu moja mia kenda tisini na tano (1995), Jhpiego ilianza masomo ya upelelezi ikishirikiana na chuo kikuu cha Zimbabwe kutafuta hiari ya gharama ya chini badala ya upimaji wa saratani ya uke inayoweza kufanya uzuiaji wa saratani ya shingo ya kizazi iwezeke katika mahali pasipo mitaji. Kulingana na matokeo ya upelelezi huo, Jhpiego ilisaidia kuunda Mrengo wa Uzuiajo Saratani ya Shingo ya Kizazi (ACCP) na kupokea posha kutoka Wakf wa Bill & Melinda Gates kuvimbisha programu ya saratani ya shingo ya kizazi. Kutoka wakati huo, Jhpiego imeendeleza na kuelekeza utaratibu wa ziara moja tu hospitalini ambapo wanawake wanapimwa na kutibiwa.

Mwaka wa elfu moja mia kenda tisini na tano (1995), Jhpiego ilianza kusimulia juu ya Virusi Vya Ukimwi/Upungufu wa Kinga Mwilini (VVU/UKIMWI) ikiunganisha na huduma za upangaji uzazi. Baada ya miaka sita, Jhpiego ilianza ushauri hiari na pimo ya bure kwa Virusi Vya Ukimwi (HIV) ikishirikiana na Mradi wa Maendeleo ya Kimataifa ya Udharura wa Marekani (MKUM) nchini Jamaika. Mwaka wa elfu mbili na mbili (2002), Jhpiego ilipata posha ya kwanza kutoka Shirika la Marekani la Ulinzi na Uzuiaji wa Magonjwa (CDC) kuendeleza kazi ya Virusi Vya Ukimwi/Upungufu wa Kinga Mwilini (HIV/AIDS), na mwaka uliofuata, ikakuza kifurishi cha somo la ulimwengu cha uzuiaji wa uambukizo kutoka kwa mama hadi mtoto wa Virusi Vya Ukimwi (HIV) ikishirikiana na Shirika la Marekani la Ulinzi na Uzuiaji wa Magonjwa (CDC), Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na washirika kutoka vyuo vikuu. Pia, mwaka wa elfu mbili na tatu (2003), Jhpiego ilikuza kifurushi cha ulimwenguni cha masomo juu ya utahirisi kukinga Virusi Vya Ukimwi (HIV) pamoja na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na pia Mradi wa Maendeleo ya Kimataifa ya Udharura wa Marekani (MKUM).

Njia ya Kuzidi Kuendelea

Dhima ya Jhpiego kazini ya afya ya mama na watoto imevimba sana, mkazo ukiwa wauguzi na wakunga wawe watunzi umeongezeka. Kutoka mwaka wa elfu moja mia kenda tisini na nane (1998) hadi leo, Jhpiego iemeongoza miradi mitatu ya ulimwengu ya Mradi wa Maendeleo ya Kimataifa ya Udharura wa Marekani (MKUM) programu ya MNH, ikifutwa na programu ya ACCESS zote mbili zikiangalia kwa makini afya ya mama na watoto wachanga - Mpango wa Shirika la Afya ya Kina Mama na Watoto (MCHIP), shirika ambalo huangalia kwa makini afya ya mama, watoto wachanga na watoto kwa jumla.

Watalaamu wa ufundi wa Jhpiego - kwa eneo la elimu ulimwenguni: upangaji uzazi/afya ya uzazi/saratani ya shingo ya kizazi; afya ya mama, mtoto mchanga na watoto kwa jumla, ushauri, tathmini, na upelelezi; kupa nguvu mifumo ya afya; Virusi Vya Ukimwi/Upungufu wa Kinga Mwilini (HIV/AIDS) na magonjwa yanayoambukiza, chapisho na udhibiti wa maarifa – wanafufua jitihada zao kuganda na kueneza magunduzi ya kufaa na ya gharama ya chini yatakaonufaisha afya ya akina mama na jamii zao.

Kama Jhpiego yaendelea mbele, wafanya kazi wataendelea kuitikia mahitaji ya washirika na wataendelea kuuliza: tunawezaje kuokoa maisha zaidi?

Haki © 2000 Jhpeigo ni shirika la chuo kikuu cha Johns Hopkins. Haki zote zimewekwa

Sera ya tovuti  | Ramani ya tovuti | Maoni