Kifua kikuu

Theluthu moja ya watu wa dunia wameambukizwa na Mycobacterium Tuberculosis, kiini kinachoambukiza kifua kikuu (TB). Mwaka wa 2007, kulikuwa na visa milioni 9.3 vya kifua kikuu ulimwenguni, asilimia themanini (80%) vikiwa viko katika nchi 22. Ijapokuwa  huduma za upimaji na matibabu ya kifua kikuu zimeunganishwa na utunzi wa afya ya msingi katika nchi nyingi, vifo kutokana na kifua kikuu viko juu – milioni 1.3 mwaka wa 2007.

Baadhi ya nchi ambazo zina wingi wa visa vya kifua kikuu, 14 ziko Afrika. Hii ni kwa sababu ya Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV) – asilimia arobaini (40%) hadi hamsini (50%) ya watu walioambukizwa na Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV) wanapata kifua kikuu maishani mwao. Kwa hakika, asilimia ishirini na tatu (23%) ya karibu vifo milioni 2 vya Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV) mwaka wa 2007 vilitokea kwa sababu ya kifua kikuu.

Jhpiego Nafanya nini

Jhpiego, shirika la kimataifa la afya linaloshirikiana na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, limetambuliwa kuwa kiongozi duniani kwa kutia nguvu mifumo ya afya katika makao wasio na mitaji mingi. Ikitumia miradi yenye uzushi, Jhpiego inatumia matokeo ya uchunguzi kuenedeleza afya ya akina mama na jamaa zao katika maeneo ya ufundi wa afya ya akina mama na watoto wachanga, upangaji familia na afya ya uzazi, na kuzuia na kutibu magonjwa wanayoambukiza. Jhpiego inafanya kazi na nia ya kukomesha kufua kikuu (TB) ulimwenguni.

Kifua kikuu ni sababu tangulizi ya vifo vya watu wanaoambukizwa na HIV. Wale ambao wana Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV) wana hatari ya asilimia kumi (10%) ya kupata kifua kikuu (TB) ikilinganishwa na asilimia kumi (10%) ya hatari kwa wale wasio na Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV). Jhpiego imeaminisha kuunganisha kifua kikuu (TB) na miradi ya Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV) ilikuendeleza maisha ya akina mama na jamaa zao kupitia uzuiaji, utunzi na matibabu ya kifua kikuu (TB). Ikiwa mshirika mkuu kufanya kazi na Mpango wa Raisi wa Dharura wa Msaada wa UKIMWI (PEPFAR), Jhpiego inafanya kazi na wizara za afya, miradi ya kitaifa ya kifua kikuu (TB) na Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV), vyuo vya elimu na mashirika wasiokuwa ya serikali kufanya kazi ya miradi ya kifua kikuu (TB) na Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV). Mwaka wa 2008, Jhpiego ilijiunga na Ushirikiano wa Kukomesha Kifua Kikuu, nia yake ikiwa kukomesha kifua kikuu (TB) ugonjwayulio tatitzo ya afya ya umma.

Malengo ya Dunia

Lengo la Maendeleo ya Milenia  la 6

Kupigana na Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua /Upunguvu wa Kinga Mwilini (HIV/AIDS), malaria na magonjwa mengine:

  • Lengo la 6c: komesha na kuanza kupindua tukio za malaria na magonjwa mengine makubwa.
  • Kionyesho 6.9: tukio, wingi na vifo vya kifua kikuu (TB)
  • Kionyesho 6.10: kadiri ta visa vya kifua kikuu vinagunduliwa na kutibiwa chini ya mradi wa kuchunguzwa mara moja na kutibiwa kwa muda mfupi (DOTS)

Malengo ya washirika wa kukomesha kifua kikuu (TB)

  • Kiwango cha uvumbuzi wa visa ni asilimia sabini (70%)
  • Mafanukio ya matibabu yako asilimia themanini na tano (85%)
  • Mwaka wa 2015: mzigo wa dunia wa kifua kikuu utapunguzwa kwa asilimia hamsini (50%) kuwa sawa na miaka ya 1990s
  • Mwaka wa 2050: visa via kifua kikuu duniani vitakuwa chini ya kisa kimoja kwa watu milioni moja kila mwaka

Mafanukio ya Nchi

Mafanukio haya yaonyesha maarifa ya Jhpiego kuendeleza miradi ya kifua kikuu (TB) katika nchi ambazo zimechaguliwa

Kenya:

  • Uongezeko wa mimba una ongeza hatari ya kuambukizwa na kifua kikuu (TB), matukio mabaya yawezekana kwa sababu ya kifua kikuu wakati wa uja uzito kwa mama na mtoto kabla ya kuzaliwa. Kama mshirika mkuu wa mradi wa Mashariki wa UKIMWI, Idadi ya watu Kipangama cha Usaidizi wa Afya Bora (APHIA II) uliofadhiliwa na Wakala wa Marekani wa Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Jhpiego imeongeza upimaji wa kifua kikuu na uhusiano katika mpango wa mafunzo wa Kaza ya Huduma kwa Waja Wazito
  • Jhpiego inasaidia utetezi, ushirikiano na ukusanyiko wa watu kupitia mafunzo wa watoaji na jamii kuzuia kifua kikuu (TB) upimaji na uzuiaji. Kwa mfano, Jhpeigo inasaidia utoaji wa huduma katika magereza kwa kufunza wenzi kutegemeza matibabu, mageuko ya maofisa wa gereza na pia wafungwa kuwa nyeti, kuongeza uwezo wa maabara, kutoa tegemezo ya zahanati na kuunganisha huduma za kifua kikuu (TB) na Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV).

Msumbiji

  • Ikiwa na fadhili kutoka Vituo vya Kudhibitisha na Kuzuia Magonjwa  Marekani (CDC), Jhpiego inatoa usaidizi wa ufundi kwa Wizara ya Afya kuendeleza mpango wa miaka mitano wa kuzuia uambukizo wa kifua kikuu (TB), pamoja na utayarishaji wa mpango wa miaka miwili wa vitendo.
  • Jhpiego pia inasaidia Wizara ya Afya kuendeleza na kuanza mpango wa mafunzo ya kuzuia maambukizo ya kifua kikuu wa kitaifa na itasiaida Wizara ya Afya na mafunzo ya watoaji huduma.

Afrika Kusini

  • Nchini Afrika Kusini, Jhpiego inajenga uwezo wa washirika wa janibu kutoa miradi unganishwa ya wema kazini ilio ya cheo cha juu, ikiwemo ushauri na upimaji wa Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV) na upimaji wa kifua kikuu (TB).
  • Jhpiego inatoa usaidizi wa ufundi kwa vyo vya masomo uya ukunga kuhakikisha ya kwamba wahitimu wanaweza kutoa huduma zinazounganishwa za kufua kikuu (TB) na Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV).

Zambia

  • Jhpiego inaendeleza mpango wa mafunzo wa kazini wa ujifundishaji  kupima na kusimamia fursa za maambukizo, pamoja na kifua kikuu (TB).
  • Kuendeleza ubora wa huduma, Jhpiego inafanya kazi na Kikosi cha Ulinzi cha Zambia kuanza mradi wa usimamizi wa viwango vya msingi na utambulisho kwa uzuiaji, utunzi na matibabu ya kifua kikuu (TB) na Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua  (HIV).

Haki © 2000 Jhpeigo ni shirika la chuo kikuu cha Johns Hopkins. Haki zote zimewekwa

Sera ya tovuti  | Ramani ya tovuti | Maoni