Saratani ya shingo ya kizazi
Jhpiego inafanya kazi ya kimataifa ili kuboresha afya ya kina mama, na njia ambazo watoa huduma za afya wanavyoelimishwa na kupewa maagizo na hatua muhimu za kutoa huduma za afya. Uzuiaji wa saratani ya kizazi hasa ni mpango unaohitaji kuhamasishwa.
Uhusiano kati ya saratani za kizazi nakutoendelea una uzito zaidi ya vile unvyodhaniwa. Zaidi ya gharama ya matibabu na kupoteza ruzuku, ugonjwa huu pia kwa njia isiyo ya kiwazi hupunguza maendeleo. Ulimwenguni, saratani ya kizazi ndio ugonjwa wa pili wa seratani ulioenea zaidi katika wanawake na unaowauwa wanawake walio na sarakasi kwa wingi katika nchi zinazoendelea. Wanawake wengi wanaofariki wamo katika miaka ya mwishoni ya 30 na miaka ya 40. Bila ya kuwa na mama, afya ya familia, hasa watoto, inaadhirika vikali. kifo cha mama kawaida huanzisha hatau chache za kijamii za kuelimisha kila mtoto, na watoto walioachwa huwa na ongezeko la kutoshughulikiwa kabisa.
Njia muhimu ikizingatiwa ili kuzuia ugonjwa huu wa saratani ya uzazi,ugonjwa mmoja wa magonjwa ya zinaa (STIs) ulio hatari zaidi duniani, itamaanisha kuboresha maisha ya maelfu ya wanawake na familia zao kila mwaka. Na tiba mpya, iliyo katika hospitali za kawaida inammanisha hatuhitaji kungojea chajo—huu ni ugonjwa mmoja ambao tunaweza kuanza kuumaliza kwa kutumia teknolojia tuliyo nazo tayari.
VIA, inayomaanisha ukaguzi wa mfuko wa uzazi, baada ya kutumia acidi siki (vinegar) iliyoongezwa maji na kupakwa kwenye mfuko wa uzazi, hii ni moja wapo wa njia rahisi za kupima saratani ya kizazi. JHPIEGO imeonyesha kuwa VIA ni njia rahisi na nyeti ikilinganishwa na ile ya "Pap smears", kwani ina matokeo ya haraka na yaweza kutekelezwa na wauguzi. Kugundua njia mpya itakayoweza kutumiwa kote ulimwengu kutibu saratani ni sehemu moja tuu inayohitajika kuumaliza ugonjwa huu. Hata hivyo, ni muhimu kuunganisha njia hii na matibabu yaliyobainishwa. Kwa bahati nzuri, "Cryotherapy"
(kukausha kiungo cha kizazi kisicho cha kawaida na "coolant" ya maji kama vile "carbon dioxide") imetumiwa na kuwa na mafanikio kwa muda zaidi ya miaka 40 kwa kutibu "dysplasia" ya kizazi. Tukiunganisha tiba ya VIA na njia hii ambayo siyo ya gharama ya juu, ambayo wauguzi wanaweza kutoa kwa urahisi, inamanisha kuwa kutakuwa na mipango itakayoanzishwa, isiyo ya gharama kubwa ya kupambana na ugonjwa huu na mipango itakayoweza kuwafikia watu wote hata walio katika nchi zilizo maskini.
Ni Yapi Yanoyoweza Kufanya kwa Sasa?
Kupunguza matukio ya saratani ya kizazi yaweza kuwa njia moja muhimi ya kuendeleza nchi na kumaliza umaskini. Mbona hatuoni haya yakitokea? Hadi hivi karibuni, sababu ilikuweko kutokuwepo kwa njia iliyo ya bei nafuu ya kupima ili kuugundua ugonjwa huu katika nchi zinazoendelea ambapo vipimo vya "Pap smears" havipatikana kwa urahisi, hasa kwa wanawake wanaoishi kwenye vijiji zisivyo na madaktari.
Jhpiego Yaingilia Kati
Katika mwanga wa tatizo hili, Jhpiego, kwa ufadhili wa Shirika la Bill na Melinda Gates, kupitia Muungano wa Kuzuia Saratani ya Uzazi (Alliance for Cervical Cancer Prevention -ACCP), imeonyesha kuwa "mbinu ya ziara mmoja (“single visit approach” -SVA) inayojumuisha VIA ikifutwa na matibabu ya "cryotherapy" (au rufaa ikiwa muhimu) ni salama,ya kukubalika na yenye upembuzi mwakinifu, katika sehemu yenye kiwnago cha rasilimali ya chini kama vile vijiji vya Thailand. Matokea haya yameongezea haja ya kutaka kufahamu mbinu hii kama mfumo wa kutumiwa kutatua matatizo ya kizahanati katika mataifa duniani. katika Jhpiego, hatua inayofuata ni ya kutafsiri matokeo kutoka kwa miradi hii na kuitekeleza katika mipango ya juhudi hizi.
Ziara ya matibabu yote kwa wakati mmoja katika nchi 20 maskini katika bara la Afrika na lile la Asia itagharimu $11 pekee kwa kila mtu maisha yake yaliyo-okolewa. Linganisha haya na ukweli wa kuwa saratani ya kizazi ndiyo inayowaangamiza wanawake wengi zaidi katika nchi hizi, na kwa hivyo umuhimu wa kuzuia ugonjwa huu utakuwa na manufaa zaidi kwa jamii kifedha na pia kimaisha.
Jhpiego imejitolea kutoa miradi na mbinu za kuzuia ugonjwa huu kwa kutumia vipimo vilivyo virahisi na pia taratibu za matibabu popote duniani. Juhudi za kuzuia saratani ya kizazi zina uwekaji katika binadamu, uchumi wa kimataifa, na manufaa ya watu wenyewe binafsi.
Wa miaka 35, Jhpiego imejitolea kuendeleza afya ya wanawake na familia kote duniani. Jhpiego imejitolea kwa ubora—kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa ni za hali ya juu na pia kuendeleza uwezo wa binadamu. Kama mshiriki wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, Jhpiego inatumia maarifa ya muda mrefu ya Chuo hiki Kikuu ili kutoa majibu yanoyotokana na maswala ya mahitaji ya huduma za afya katika dunia ya leo.







