Sisi Ni Nani
Jhpiego ni shirika lisilo la faida la kimataifa linalo shirikiana na chuo kikuu cha Johns Hopkins. Jhpiego imefanya kazi kuzuia vifo vya bure vya wanawake na jamii zao zaidi ya miaka thelathini na tano katika nchi mia moja hamsini.
Jhpiego inafanya kazi na watalaamu wa afya, viongozi wa serikali na jumuiya kupa uangalizi wa kiwango cha juu kwa wananchi wao. Jhpiego inaendeleza mikakati kusaidia nchi kujisaidia kwa kufunza watoaji wa utunzaji afya wenye maarifa, kutia nguvu mifumo ya afya na kuboresha jinsi ya kutoa utunzaji.
Jhpiego inabuni na kufumbua njia jipya za kufaa na za gharama ya chini kuhifadhi ubora wa uangalizi wa wakina mama na jamii zao. Maamuzi haya ya kufaa na yenye ushahidi yanavunja vizingiti zinazozuia utoaji wa afya wa cheo cha juu kwa wale wanadhuriwa duniani.
Ujumbe na Thamani
Jhpiego imeweka wakf kuboresha afya ya wakina mama na jamii katika nchi zinazoendelea. Tangu awali yetu kama watalaamu wa mifumo ya uzazi, afya ya mama na watoto, Jhpiego ina kumbatia changamoto mpya ikiwemo Virusi Vya Ukimwi/Upungufu wa Kinga Mwilini(HIV/AIDS), malaria, uzuiaji saratani ya shingo ya kizazi na afya mijini – kuonyesha uungano zaidi wa afya ulimwenguni. Tunachukua ujuzi wa kisasa wa sayansi na teknolojia, kuutumia kuendeleza utatuzi wa kufaa na za gharama ya chini na kuzifaidi kutoka nyumbani hadi hospitalini, kijiji hadi mjini.
Jhpiego inasaidia nchi shirika kutatua mahitaji ya afya ya wanawake na jamii zao. Tunafanya kazi hii kwa kufunza na kutayarisha watoaji utunzi wa afya (madaktari, wauguzi, wakunga na watoaji utunzi wa jumuiya) kutumia maarifa yanayofaa kupaa utunzaji afya wa cheo bora. Jhpiego huamini kwa vile watu wengi hawawezi kupata huduma rahisi, ni lazima huduma zipelekwe kule wanaokaa na pia kwa jumuiya.
Kustahili haja hii, Jhpiego inabuni na kutumia njia za utoaji utunzi wa afya za gharama ya chini ambazo zinaweza kupelekwa na watoaji utunzaji wa afya wa jumuiya nyumbani au na daktari ama mwauguzi hospitalini. Tunategemeza na kuunganisha huduma na maumizi ya utunzi wa afya ili kutibu majonjwa mbalimbali na wanawake na jamii watibiwe hali kadha wa kadha pahali pamoja.
Tunajenga uwezo wa kutia nguvu mifumo ya afya ya jumuiya kupitia uteteji, endelezo ya sera na njia za maendeleo ya vitendo. Mwishoe, kikomo cha Jhpiego ni fululizia – kuacha nyuma wavu ya watoaji utunzi wa afya mwema na kujenga msingi wenye nguvu ya kutumia tutakapoondoka.







