Upangaji Uzazi/Afya ya Uzazi

Upangaji Familia Unatia Nguvu Wanawake Kuchagua Chaguo Zinazookoa Maisha

Kila siku, wanawake ambao wanaweza kupata huduma za upangaji familia (FP) wana nguvu kuchagua hiari kama kuchelewesha umama, kupanga mimba na kuzuia mimba zisizitakikana na kutoa mimba. Kila mwaka, wanawake wanachagua hiari hizi na kupanga jamaa zao ilikuzuia vifo moja kwa tatu vya akina mama na zaidi ya vifo milioni 2 vya watoto wachanga na watoto kwa jumla. Walakini, maisha zaidi yangeokolewa. Ijapokuwa maendeleo ya teknolojia ya kufaa na ya bei stahili yameonekana, kadiri wanawake milioni 200 na waume na wake milioni 120 wanaohitaji huduma za upangaji familia bado hawana njia ya kuzipata.

Jhpiego Inafanya Nini

Kwa kuunganisha upangaji familia (FP) na baadhi ya huduma za afya ya uzazi (RH), Jhpiego imeweza kuleta njia za uzuiaji za kisasa na huduma zingine za muhimu za upangaji uzazi karibu na wanawake wanaozihitaji. Wanawake wa umri ya kuzaa wanahitaji maarifa ya hiari za uzuiaji, kupanga mimba na huduma za upangaji familia. Jhpiego inachukua kila na fursa kutoa maarifa haya muhimu kwa wanawake wote wanaohudhuria huduma kwa waja wazito na kujifungua katika kituo, wanatumwa kupata huduma za utunzi wa haraka au kupata huduma za baada ya kujifungua.

  • Upangaji familia (FP) na utunzi baada ya kujifungua -Wanawake baada ya kujifungua wanahitaji kujua masilahi ya kupanga mimba kwa ajili ya afya yao na afya ya mtoto, na ya kwamba inawezekana kushika mimba kabla ya hedhi. Ikiwa hawanyonyeshi, urutubaji waweza kurudi baada ya wiki sita baada ya kujifungua. Nchini Kenya, ikiwa na usaidizi wa mradi wa Ufikivu wa Huduma za Zahanati na Jamii ya Uzazi, Afya kwa Akina Mama na Upangaji Familia (Access-FP), serikali imeimarisha huduma za baada ya kujifungua kwa kudhihirisha upangaji familia (FP). Mradi wa Ufikivu wa Huduma za Zahanati na Jamii ya Uzazi, Afya kwa Akina Mama na Upangaji Familia (ACCESS-FP) iliendeleza mpango wa upangaji familia baada ya kujifungua wa kwanza wa nchi ya Kenya, uliotumiwa kufunza watoaji huduma 98. Kupitia mradi wa Ufikivu wa Huduma za Zahanati na Jamii ya Uzazi, Afya kwa Akina Mama na Upangaji Familia (ACCESS-FP), zaidi ya wanawake 11,700 wamepata huduma wakati wa ziara moja ya baada ya kujifungua zilizokuwa pamoja na huduma za upangaji familia (FP) na ushauri.
  • Upangaji familia na utunzaji baada ya uavyaji mimba (PAC)– urutubaji wa mwanamke unaweza kurudi baada ya wiki mbili baada ya uavyaji mimba au  kuharibika mimba. Kwa hivyo ni muhimu wanawake wanaopata utunzaji baada ya uavyaji mimba (PAC) kuondoka zahanati wakiwa na njia za kuzuia mimba za kisasa na maarifa ya upangaji familia (FP). Kwa kutoa ushauri wa upangaji familia na uzuiaji wa kufaa wakati wanawake wanapata huduma za utunzaji baada ya uavyaji mimba, watoaji wanaweza kusaidia wanawake kuepuka mviringo wa hatari wa mimba zisizitakikana na uavyaji mimba.
  • Upangaji familia na upimaji saratani ya shingo la kizazi – baadhi ya visa vyote vya saratani zote za shingo ya kizazi, asilimia themanini na tatu (83%) zinafanyika katika nchi zinazoendelea. Kuunganisha ziara moja rahisi ya upimaji na matibabu na kiteknolojia pamoja na programu za upangaji familia (FP) zilizoko ya weza kuwa na athari kwa afya ya wanawake wa nchi zinazoendelea. Tena, kuunganisha upangaji familia (FP) na mipango ilioko ya kupima saratani ya shingo ya kizazi ya weza kutanua upataji wa huduma muhimu kwa akina mama. Nchini Guyana, Jhpiego inatafuta fursa  za kuunganisha huduma za ufundi za upangaji familia na programu zilizopo za mafunzo ya saratani ya shingo ya kizazi ili watoaji huduma watoe huduma za upangaji familia kwa washiriki wanaopimwa saratani ya shingo ya kizazi.
  • Upangaji familia (FP) na ushauri na upimaji Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua HIV- washirika wanaotafuta huduma za ushauri na upimaji wa  Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV)(HCT) na washirika wanaotafuta huduma za upangaji familia ni wale wale tu, na mara nyingi ni wanawake. Washirika, watoaji na programu , wote wanaweza kupata faida kutoka uunganisho wa huduma hizi mbili. Kwa mfano, kwa kuzuia mimba zisizopangwa na mimba zisizo rai miongoni mwa wanawake walio na Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV), upangaji familia unapunguza Uzuiaji wa Uambukizaji Kutoka kwa Mama hadi Mtoto Uzuiaji wa Uambukizo kutoka Mama hadi Mtoto (PMCT) ya Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV). Nchini Uhabeshi, Jhpiego inafanya kazi na Taasisi ya Gates na shirika la Kimataifa la Pathfinder kutoa ushauri na huduma za upangaji familia kwa washiriki wanaotaka huduma za ushauri na upimaji wa Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV)(HCT). Tunafanya kazi na wenye fungu kuendeleza agizo za ushauri wa upangaji familia (FP) na usaidizi wa kazi wa watoaji huduma za ushauri na upimaji wa Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV)(HCT). Kwa kutumia zana hizi, watoaji wanaweza kutoa huduma ifaavyo ilikujali mahitaji ya washirika walio na Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV).
  • Upangaji familia (FP) na utunzi wa afya ya watoto– wanawake wasiojitafutia utunzi wa baada ya kujifungua wanaweza kufikiwa wakati wa ziara za utunzi wa watoto (kwa mfano, chanjo za watoto wachanga). Kwa kutoa mpango wa utunzi uliounganishwa wakati wa ziara za utunzi wa watoto – kuongeza taarifa ya wanawake juu ya hiari za upangaji familia na unyonyeshaji – tunaweza kufikia wanawake ambao wanapitwa na fursa hii kuepuka mimba zisizopangwa.

Viwango muhimu vya utoaji huduma za upangaji familia (FP) na afya ya uzazi (RH)

Ubora na upatikanaji wa huduma za upangaji familia na afya ya uzazi unategemea sera, kanuni na miongozo ya kitaifa ya ustahiki na ya kisasa. (Mpaka leo, Jhpiego imeendeleza na kueneza miongozo ya kitaifa ya upangaji familia na afya ya uzazi katika nchi 25.) Zaidi, utoaji huduma za cheo cha juu za upangaji familia na afya ya uzazi unahitaji njia yenye nguvu kusaidia mifumo ya elimu wa kabla ya na baada ya kuanza kazi. Mifumo hii nayo hutoa na hutegemeza kundi la wafanyikazi lenye nguvu. Jhpiego inafanya kazi ya washirika wa ndani ya nchi kuhakikisha ya kwamba viwango hivi viko na vina nguvu na ni vya kisasa inavyohitajika.

Kaza nyingine ya afya ya uzazi (RH): uzuiaji saratani ya shingo ya kizazi (CECAP)

Kila mwaka, karibu visa 493,000 vipya vya saratani ya shingo ya kizazi huonekana na karibu wanawake 274,000 wanakufa kutokana na ugonjwa huu. Lakini, mbalimbali na saratani zingine, saratani ya shingo ya kizazi inaweza kuzuiwa. Ikiwa na ushirikiano na wenye fungu na washirika, Jhpiego imeanza mradi wa ziara moja (SVA) – mradi wa kipekee, usio na hatari kwa matibabu, unaokubalika na wa kufaa sana wa kuzuia saratani ya shingo ya kizazi katika makao yasio na mitaji. Mradi wa ziara moja (SVA) ni uchunguzi wa moja kwa moja wa shingo ya kizazi kwa asidi asetiki (VIA) kuvumbua vidonda vya saratani katika shingo ya kizazi, ikifuatiwa na utoaji wa matibabu kutumia sairotherapi wakati wa ziara moja.

Kumulika Mradi: Jhpiego Hutegemeza Utatuzi Unaundwa na ni wa Janibu katika Mitaa Michafu ya Nyumba Mbovu

Changamoto za kawaida za afya zinapatikana katika mitaa michafu ya nyumba mbovu duniani. Tangu mwaka wa 2004, katika mitaa michafu ya nyumba mbovu ya Nairobi nchini Kenya, Jhpiego inatia nguvu bidii kumiliki afya ya jamii. Jhpiego inafanya kazi na wafanyikazi wa afya na jamii ilikufikia nia; wote katika mitaa michafu ya nyumba mbovu kupata huduma bora za upangaji afya (FP) na afya ya uzazi (RH).

  • Wenye fungu wamekutana kupata maarifa kutoka jamii, wafanyikazi wa afya na mashirika ya serikali ambayo husimamia vituo vya afya.
  • Usaidizi wa mafunzo na usimamizi umetia nguvu uwezo wa wasimamizi. Sasa, watoaji utunzi wa afya wanatoa huduma za cheo cha juu, na watoaji na wasimamizi wanaweza kujenga uhusiano na washiriki na watoaji.
  • Ujuzi na maarifa ya watoaji utunzi wa afya umeendelea katika maeneo kama teknolojia ya uzuiaji na uunganisho wa upangaji familia (FP)/ Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua (HIV).
  • Wafanyikazi wa kijamii wa kujitolea wamefunzwa kutoa usaidizi na ushauri kwa jamii wanaohitaji huduma za upangaji familia (FP)/afya ya uzazi (RH).

Mpaka leo, zaidi ya watu 50,000 wamefikiwa kupitia mafunzo: katika upangaji familia (FP)/afya ya uzazi (RH) – watoaji 276; katika utoaji wa afya ya uzazi na utoaji wa vidonge na kondomu – wafanyikazi 268 wa jamii; na kwa mambo mengi ya afya ya jamii – viongozi 438 wa jamii. Zaidi, miendo ya upangaji familia kukubaliwa imeongezeka sana. Kati ya Mei mwaka wa 2007 hadi Oktoba mwaka wa 2008, kwa mfano, uzuiaji wa tembe kupokewa uliongezeka na asilimia mia ishirini na tatu (123%) na upokeaji wa kifaa cha mfuko wa uzazi wa ndani (IUD) uliongezeka kwa asilimia mia moja arobaini na sita (146%).

Haki © 2000 Jhpeigo ni shirika la chuo kikuu cha Johns Hopkins. Haki zote zimewekwa

Sera ya tovuti  | Ramani ya tovuti | Maoni