Uzuiaji na Ulinzi wa Miradhi

Kwa zaidi ya muongo mmoja, Jhpiego imekuwa kiongozi wa kimataifa katika kutetea na kutekeleza viwango vinavyo tokana na ushahid kutoka kwa msingi kwa ajili ya kuzuia maambukizi "infection prevention (IP) " mazoea ambayo kuwakinga mteja na mfanya kazi wa kutoa huduma za afya, na imeendeleza na kutekeleza juhudi katika zaidi ya nchi 40.

Matumiaji ya njia sahihi za IP:

  • Hupunguza hatari ya kuambukiza na kuwasambazia wateja magonjwa
  • Huzuia watoa huduma hizi za  afya katika ngazi zote  kutoka kwa hatari ya kufiduliwa na magonjwa ya kuhatarisha maisha
  • Huendeleza matumizi mbora ya usimamizi wa takataka ili kupunguza maambukizo kwa jamii
  • Hupunguza uchafuzi wa mazingira kwa njia ya matumizi sahihi ya utaratibu wa kuziunda tena vitu vilivyo tazamiwa kutumiwa mara moja pekee

Kwa kuunganisha kwa taratibu IP katika juhudi za huduma za afya kama vile mpango wa uzazi, afya ya uzazi, afya ya wajawazito na watoto wachanga, na miradi ya kuzuia Virusi vya Ukimwi/UKIMWI, nchi zinaweza kupunguza kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza na pia kupunguza hatari ya kuambukizwa Virusi vya Ukimwi/UKIMWI kwa watoa huduma hizi za afya. Maoni yaliyobadilika kuhusu hatari hizi husaidia kupunguza kujiuzulu kwa wafanya kazi wa huduma za afya na huongezea uwezekano wa kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi watakaokamilisha elimu ya msingi ili wawe madaktari, wauguzi, wakunga na wafanyakazi wa aina zote za huduma za afya.

Mambo kadhaa ni muhimu katika muelekeo wa Jhpiego ili kuhakikisha njia zilizo sahihi:

  • Maendelezo ya  kitaifa kuhusu miongozo na viwango vya IP yaliyotokana na mazoea bora yaliyothibitishwa
  • Maendelezo na matumizi ya rejea na vifaa vya kufundisha IP zilizolingana na viwango vya kimataifa
  • Maendelezo ya miongozo ya kitaifa ya kufunza, na miongozo maluum iliyotokana na  kukabili matukio yanayotoka kwenye mitaa (site-specific) na inayotumia viwango vya kimataifa
  • Maendelezo ya  viwango vinavyosaidia utekelezaji wa IP na utekelezaji wa viwango hivi kwa njia ya utekelezaji wa taratibu inayo boresha mchakato huu na inayohusisha ushirikiano wa wafanyakazi wote
  • Kutumia vifaa visivyo ghali, na vinavyopatikana kwenye mitaa (kama vile ndoo za plastiki, "bleach" na jiko (steamers) zinatomika huko Asia kwa kupika) ili kupunguza gharama inayohusika na IP na kuondoa vikwazo vinavyo zuia uboreshaji wa huduma za afya.

Hatua za Jhpiego

Chapisho la mwongozo wa IP la Jhpiego la hivi karibuni, "Infection Prevention Guidelines for Healthcare Facilities with Limited Resources", linatoa mwongozo kwa hospitali na vituo vingine vinavyotoa huduma zingine za jumla, matibabu, upasuaji na huduma za "obstetric". Mwongozo huu unaongezewa na rasilimali nyingine ya kijitabu cha kujifunza kilichoundwa kutoa elimu ya msingi inayohusiana na IP na ujuzi katika ngazi zote za watoa huduma za afya katika kozi inayochukua siku sita. Kozi hii yaweza kufunzwa kama mafunzo ya kikundi, kuchukuliwa pia kwa kujifunza kibinafsi moja-kwa-moja, au kuunganishwa na  mitaala ya mafunzo mengine katika elimu ya huduma  za zahanati ya wale ambao hawajahitimu bado ikiwa ni pamoja na afya ya wajawazito/watoto, "obstetrics/gynecologia" afya ya jamii, matibabu na afya ya familia, na upasuaji kwa jumla.

Kuna video mbili zinazopatikana ili kutumika kwa mafunzo haya yaliyo katika kijitabu hiki—"Infection Prevention for Healthcare Facilities with Limited Resources: Overview and Practical Training Demonstration Segments and Safe Practices in the Operating Room". Zinaelezea umuhimu wa mazoea ya IP katika kuwakinga wateja na watoa huduma za afaya, na huonyesha hatua zilizo muhimu za kutayarisha vyombo vya usindikaji. Mafunzo ya Jhpiego ReproLearn® tutorial (kwenya CD-ROM na kwenye Mtandao), sehemu ya pili ya mfululizo wa “Huduma za Wanawake Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi/UKIMWI katika rasilimali zilizo na vipimo" inaelezea hatari ya kupata Virusi vya Ukimwi na magonjwa mengine katika mazingira ya kutoa huduma za afya na inapitia mazoea ya IP ili kufanya mahali pa kazi pawe salama.

Kwa miaka 35, Jhpiego Imejitolea kuimarisha afya ya wanawake na familia duniani kote. Jhpiego imejitolea kwa ubora—kuhakikisha utoaji bora wa huduma ya hali ya juu na pia kuimarisha maendelezo ya uwezo wa binadamu. Kama mshirika  na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, Jhpiego hutumia  kina  kikuu cha utaalamu cha Chuo hiki Kikuu ili kuendeleza  majibu kwa maswala na changamoto za mahitazi ya afya ya uzazi katika dunia ya leo.

Haki © 2000 Jhpeigo ni shirika la chuo kikuu cha Johns Hopkins. Haki zote zimewekwa

Sera ya tovuti  | Ramani ya tovuti | Maoni