Uzuiaji na Utunzaji wa Malaria
Ugonjwa wa kuambukiza wa Malaria, husambazwa na mbu na ni mojawapo wa tatizo kubwa la afya kimataifa. Kila mwaka, kuna kesi kati ya milioni 350–500 za malaria duniani-kote na angalau vifo milioni ; na 90% ya kesi hizi hutokea Afrika.
Wanawake wajawazito na watoto wao wachanga ndio hasa walio kwenye hatari ya ugonjwa huu. Malaria katika ujauzito huchangia anemia kali, watoto kuzaliwa na uzito wa chini na pia hudhuru mwili wa mtoto kukua vizuri. Kila mwaka, takribani wanawake milioni 50 wanaoishi katika nchi zenye kawaida ya kupata malaria duniani kote hupata mimba. Katika Afrika, karibu 10,000 ya wanawake hawa na watoto wao wachanga 200,000, hufariki kutokana na kuambukizwa malaria wakiwa na mimba.
Jhpiego Inafanyenje?
Katika kukabiriana na mgogoro huu wa afya, kazi ya Jhpiego ya malaria inalenga hatua bora zenye gharama nafuu ili kuzuia malaria katika mimba na pia kukabiliana na ugonjwa huu kwa wanawake walio wagonjwa.
Kufikia mwisho huu, Jhpiego hufuata mbinu tatu muhimu za Shirika la Afya Duniani(WHO):
- Katika maeneo imar ya mambukizi, angalau "dosi" mbili zamatibabu yanayozuia mambukizi katika mimba (IPTp) na dawa madhubuti za kupambana na malaria, kw sasa "sulfadoxine-pyrimethamine"
- Kuzidisha matumizi ya vyandarua vya vitanda vilivyotibiwa na dawa ya wadudu
- Utambuzi na usimamizi wa haraka wa ugonjwa wa malaria kwa wanawake wajawazito
Kwa vile uchunguzi unaonyesha kuwa wanawake waliohudhuria huduma zinazolenga malezi bora ya waja wazito (FANC)1wanao uwezekano zaidi wa kukaa bila ya kuambukizwa malaria na pia wanaweza kujifungua watoto wenye afya njema. Jhpiego imeanzilisha utekelezaji wa huduma za FANC katika Afrika. Mtazamo huu unahakikisha kwamba wanawake wajawazito wanapata huduma wanazohitaji kwa minajili ya kukinga na kudhabiti malaria katika ujauzito, pamoja na hatua zinginezo za kuboresha afya. Ufikiaji wa jamii ni nyezo muhimu kwa mradi wa Jhpiego kuhakikisha wanawake wanahusishwa na huduma hizi za nyakati za ujauzito.







