Uzuiaji na Utunzaji wa Virusi vya Ukimwi Vilivyopungua/Upungufu wa Kinga Mwilini

Lengo la sita la Maendeleo ya Milenia (MDG) la Umoja wa Mataifa lina wito wa kusimamisha na kupunguza kuenea kwa Virusi vya Ukimwi kufikia mwaka wa 2015, na mafanikio ya upatikanaji wa matibabu ya Virusi vya Ukimwi/UKIMWI kufikia mwaka wa 2010. Ingawaje hatua imefanyika, janga hili linaendelea  kuangamiza maisha yasiyo kiasi. Ukweli huu ni hasa kwenye nchi zinazoendelea, ambapo Virusi vya Ukimwi/UKIMWI vimeongezea mzigo mkubwa juu ya mifumo ya huduma za afya iliyo tatizika tayari na pia idadi ya watoa huduma za afya inazidi kupungua, na ambapo zaidi ya 90% ya watu walioambukizwa na  Virusi vya Ukimwi wanaishi.1 Wanawake na watoto ni miongoni ya walio kabwa kabisa, kukiwa na wanawake wa miaka 15 kuendelea wanaofikia 50% ya idadi ya watu walio ambukizwa Virusi vya Ukimwi duniani, na inakadiriwa watoto milioni 2.1 wanaishi na Virusi vya Ukimwi/UKIMWI ipatavyo mwaka 2007.2 Licha ya changamoto kama hizi, Jhpiego imejitolea kuendeleza  maendeleo thabiti, ili kupata mafanikio ya "MDG Six".

Vile Jhpiego Inavyojihusisha

Jhpiego, ambalo ni shirika la limataifa linalohusishwa na Chuo Kikuu cha John Hopkins (JHU), inatambuliwa kimataifa kama kiongozi  katika kuimarisha mifumo ya afya kwa kutoa huduma za hali ya juu kwa wanawake na familia katika mazingira yenye rasilimali ndogo. Zaidi ya miaka 13 iliyopita,Jhpiego imeleta ubunifu unaotegemea ushahidi  kwa kukinga, huduma na matibabu ya Virusi vya Ukimwi/UKIMWI na magonjwa mengine ya kuambukiza. Kama Mshiriki muhimu wa Mpango  wa Dharura wa Rais wa UKIMWI (the President’s Emergency Plan for AIDS Relief - PEPFAR)3, Jhpiego inashirikiana na wizara za afya (MOHs), miradi ya kitaifa ya UKIMWI, taasisi za elimu,mashirika yasiyo yakiserikali, na mashirika yaliyo na msingi wao kwa makanisa na jamii ili kutekeleza mipango ya Virusi vya Ukimwi/UKIMWI. Utaalamu wetu wa kiufundi wa Virusi vya Ukimwi/UKIMWI unakumbatia maswala mbalimbali ya kiufundi kama vile:

  • Uzuiaji wa maambukizo ya Virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama-kwenda- kwa mtoto(PMTCT), kushughulikia njia kuu ya maambukizo ya Virusi vya Ukimwi kwa watoto
  • Ushauri na upimaji(CT) kwa ajili ya Virusi vya Ukimwi, inayobainiwa kama mwanzo mwa njia ya makini ya kuzuia Virusi vya Ukimwi, kutoa huduma na matibabu kwa watu wanaopima kuwa na virusi, na pia kuzidisha kupunguza hatari ya maambukizi kwa wale ambao hawana virusi
  • Kupashwa tohara kwa Wanaume (MC), kumeonyeshana kupunguza hatari ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi  kutoka kwa  wake-kwenda- kwa waume na 60%
  • Kuzuia maambukizo kupitia njia ya matibabu ya Virusi vya Ukimwi na mangojwa mengine ya kuambukiza kupitia njia  rahisi za mazoea ya uzuiaji, ikiwa ni pamoja na "post-exposure prophylaxis" ya Virusi vya Ukimwi
  • Utoaji wa tiba ya kurefusha maisha (antiretroviral therapy-ART), kwa watu wazima na watoto na matibabu ya magonjwa yanayoambatana na maambukizi  na huduma maalum (palliative care), kutoka kituo cha matibabu  kueelekea kwenye  kiwango cha jamii
  • Ujumuishaji wa Virusi vya Ukimwi/UKIMWI naTB, saratani ya kizazi, malaria katika ujauzito, mpango wa uzazi na huduma za afya ya wajawazito na watoto, ili kukabiliana na tatizo la maambukizo-ya ushiriki katika  wangonjwa walio na Virusi vya Ukimwi/UKIMWI na pia kuwafikia watu wengi kama inavyowezekana.

Maelezo muhimu kwingineko kuhusu shughuli za Jhpiego na Virusi vya Ukimwi/UKIMWI

Katika mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi/UKIMWI, Jhpiego hufuata njia bora na utafiti unao kata-makali (cutting-edge) kukabiliana na mambo halisi duniani. Ili kukamilisha haya, tunatumia mbinu bunifu katika maeneo ya mipango hii kama vile kuongezea uwezo wa binadamu,utendaji na kuzidisha uboreshaji, na sera na maendelezo ya miongozo.  Hapa ni baadhi ya maelezo muhimu kutokana na juhudi zetu tunazoziendeleza kuhusu Virusi vya Ukimwi/UKIMWI:

  • Huko Msumbiji,Jhpiego na Wizara ya Afya (MOH) zinafanya kazi  kwa pamoja ili kuongezea chanjo iliyoanzishwa na mtoaji wa upimaji na ushauri nasaha (provider-initiated testing and counseling - PITC).4Ndani ya mwaka mmoja pekee, zaidi ya watu 147,000 walipimwa kutokana na matokeo ya mpango huu.
  • Jhpiego na Wizara ya Afya ya Ethiopia(federal MOH) zinatekeleza mtandao bunifu  kwa akina mama wenye Virusi vya Ukimwi. Kupitia juhudi hizi, wanachama  wanafunzwa kama "mama washauri" (“mother mentors,”) ambao hupatanisha wanawake wajawazito wanaokuja kuhudhuria shughuli ya mimba kwenye zahanati na huduma zinginezo mbalimbali za  PMTCT.
  • Tangu mradi wetu wa mwanzo wa majaribio wa MC katika mwaka wa 2003, Jhpiego  imeongoza kwenye shughuli za kuimarisha au kuongezea huduma zilizo pana za MC 5huko Zambiana Ethiopia, na imeanzisha juhudi kama hizi huko Lesotho,Botswanana Afrika Kusini.
  • Katika makazi duni  ("slums") yanayozingira Nairobi, Kenya, Jhpiego inatekeleza Mradi wa Vituo Zinazotoa Huduma Zaidi (Comprehensive Care Center Program) inayosaidia watu kwenye jamii wanaoishi na Virusi vya Ukimwi waweze kupata huduma za afya ikiwa ni pamoja na msaada wa huduma za kimwili na za kisaikolojia (physical and psychological support).
  • Huko Afrika Kusini, Jhpiego inaongoza  katika juhudi za kupanua wajibu wa wauguzi ili kuwaanzisha na pia kuwasimamia wagonjwa katika ART kupitia "kubadilishana kazi" ("task-shifting”), ili kusaidia kukabiliana na mgogoro wa rasilimali ya binadamu katika huduma za afya.
  • Jhpiego imejipa sifa za mamlaka katika maswala mbalimbali kwenye maeneo ya kliniki zinazo husiana na Virusi vya Ukimwi/UKIMWI, na kusababisha ushirikiano na mashirika kadha yenye uwezo mkubwa—ni mashirika kama vile WHO, CDC na UNAIDS na pia Ofisi ya Mratibu wa US Global AIDS /PEPFAR—kuhusu mambo ya kimataifaya Virusi vya Ukimwi/UKIMWI inayohusu miongozo , zana na rasilimali za elimu ya PMTCT, MC na HIV–CT.

Kupitia kazi yetu katika Virusi vya Ukimwi/UKIMWI, kama kawaida ya juhudi zetu zote, Lengo la muhimu zaidi la Jhpiego’s ni uendelevu, kuhifadhi mtandao ulio tayarishwa vyema wa waatalamu wa huduma za afya na pia msingi imara wa kitaasisi  ili waweze kuuendeleza wakati tutakapoondoka.

1UNICEF. 2008. The state of the world's children (Hali ya watoto wa dunia) 2007. katika: www.unicef.org/publications/index_36587.html
2UNAIDS, WHO. 2007. AIDS epidemic update ( maelezo ya Janga la Ukimwi). katika: http://data.unaids.org/pub/EPISlides/2007/2007_epiupdate_en.pdf
3Unahifadhiwa na kushirikiana na mashirika muhimu ya Kimataifa kama vile Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Merikani (USAID), U.S. Centers for Disease Control and Prevention (CDC), Global Fund for AIDS, Tuberculosis, and Malaria (GFATM), United Nations Children’s Fund (UNICEF), United Nations Joint Programme for HIV/AIDS(UNAIDS) and World Health Organization (WHO), na pia kutoka kwa mashirika na misingi ya kibinafsi kama vile GlaxoSmithKline, Pfizer, Wallace Global Fund na The Rockefeller Foundation
4katika PITC, watoa huduma hupendekeza HIV–CT kwa wateja wote kanda/wakaaji waliotambuliwa kama sehemu ya utaratibu wa huduma;    mkazo umewekewa katika ushauri, siri na ukubaliaji wa mteja.
5Ikiwa ni pamoja na huduma zingine za afya ya uzazi, kama  vile ushauri wa kupunguza hatari, uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya zinaa, nk.

Haki © 2000 Jhpeigo ni shirika la chuo kikuu cha Johns Hopkins. Haki zote zimewekwa

Sera ya tovuti  | Ramani ya tovuti | Maoni